Rais wa Yanga SC Hersi Said ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Jumapili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir utakaochezwa Tunisia wameweka bonasi za aina mbili.

Hersi amekiri kuwa katika michezo ya Kimataifa watatoa bonasi kubwa timu ikipata ushindi pamoja na kupata sare mechi za ugenini.

“Mashabiki walitaka kutuona tunaingia makundi na tumefanikisha viongozi pamoja na wachezaji, kwenye timu yetu tunatoa bonasi ya ushindi na safari hii tutatoa pia ya droo ugenini maana kupata sare mechi za ugenini pia ni sehemu ya kupata mafanikio”>>> Hersi Said Kupitia AZAM TV