Kanali Hamis Ngoi kutoka chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti akikabidhi medali ya heshima kwa Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Group Salum Khamis baada ya kutembelea kampuni hiyo ya vinywaji na kutambua mchango wa kampuni kwa jamii na maendeleo.


*****
Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Duluti Arusha kimeipongeza Kampuni ya Vinywaji ya Jambo kwa kuipatia medali ya pongezi ikiwa ni kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kujitoa kwake kwa jamii na maendeleo kiujumla.


Wakikabidhi medali ya heshima kwa niaba ya wanajeshi kutoka mataifa zaidi ya 14 Mkuu wa Kitengo cha Mazoezi na Mafunzo Duluti, Kanali Hamis Ngoi ameelezea kuwa wao kama chuo ambacho kinatoa mafunzo kwa Wanajeshi kutoka mataifa mbalimbali wamefurahishwa na aina ya uwekezaji unaofanywa na kiwanda cha Jambo na kuongeza kuwa ziara yao ya kujionea namna ya ufanyaji kazi kwa kiwanda cha Jambo imekuwa ya manufaa makubwa.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Group, Salum Khamis amewashukuru wanajeshi hao kwa zawadi waliyompatia na kuwaahidi ushirikiano kwa Chuo hicho cha Duluti wakati wote.