ELLEN WHITE PRE AND PRIMARY SCHOOL 

P. O. Box 3118, 

Nzuguni Dodoma – Tanzania 

Mob: 0769 352 215 / 0673 443 962 

Email: [email protected] 

Web: www.ews.sc.tz 

 TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA                    11/08/2023 

Utangulizi Ofisi ya Meneja wa shule ya Ellen White School- Dodoma, inapenda kuutangazia umma kuwa shule imetoa nafasi mbalimbali za ajira kama ifuatavyo:- 

1. Walezi wa Watoto (matrons/patrons) Nafasi 5 

 Waajiriwa katika nafasi hii wanatakiwa kuwa wenye sifa zifuatazo:- 

 Umri usiopungua miaka 30 na usiozidi miaka 50. 

 Mwenye Elimu ya malezi ya watoto atafikiriwa kwanza. 

 Elimu ya kidato cha nne na kuendelea. 

 Uwezo wa kuongea na kuandika lugha ya Kingereza kwa ufasaha. 

 Mwenye upendo kwa watoto na mvumilivu katika kazi ya malezi ya watoto. 

 Mcha mungu na mwenye maadili mema. 

 Mwenye uwezo wa kufundisha michezo kama sifa ya ziada lakini siyo lazima. 

 Mwenye uzoefu wa kushughulika na watoto 


2. Katibu Muhtasi (Secretary) Nafasi 2 

 Waajiriwa katika nafasi hii wanatakiwa kuwa wenye sifa zifuatazo:- 

 Elimu ya kidato cha nne na kuendelea. 

 Uwezo wa kuongea na kuandika lugha ya Kingereza kwa ufasaha. 

 Kasi nzuri ya kuchapa barua na nyaraka nyingine bila makosa.. 

 Uwezo wa kutumia vifaa vya kazi ikiwemo computer, printer, photocopy nk. kwa weledi na kuwa mtunzaji mzuri wa vifaa hivyo. 

 Mwenye uvumilivu wa kufanya kazi hata baada ya saa za kazi za kawaida. 

 Mwenye kutoa huduma nzuri kwa wateja wakati wote. 


3. Walimu Nafasi 10 

Waajiriwa katika nafasi hii wanatakiwa kuwa wenye sifa zifuatazo:- 

Wenye Astashahada (cheti) au Stashahada (Diploma) ya ualimu wa Elimu ya Msingi au elimu ya awali (Early Childhood Education). 


 Masharti ya jumla kwa kazi zote: 

 Waombaji wote waambatanishe maombi yao na vivuli vya cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha NIDA. 

 Waombaji waambatanishe maelezo yao binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani, namba ya simu ya kuaminika, pamoja na majina matatu ya wadhamini wa kuaminika. 

 Maombi yote yaambatane na vivuli vya vyeti vya taaluma (kidato cha nne, sita nk.) pamoja na picha moja ya passport iliyopigwa hivi karibuni. 

 Maombi yaandikwe kwa lugha ya Kingereza. 

Zingatia Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono na zitumwe kwenye barua pepe [email protected] au anwani tajwa hapa chini. 

NB;

Kwenye barua yako, onesha/andika  maxflix93.com  kama sehemu ulipo ona/sikia tangazo hili.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30/8/2023 muda wa saa za kazi. 

SCHOOL MANAGER 

ELLEN WHITE SCHOOL 

P.O BOX 3118 

DODOMA