Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema aliamua kunyamaza na anaendelea kukaa kimya lakini amewahakikishia Watanzania kuwa hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa la Tanzania na wala hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuiuza Nchi ya Tanzania.

Rais Samia amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Chuo cha Tumaini Makumira, Arusha leo August 21,2023.

Rais Samia amenukuliwa akisema “Ndugu zangu, na hususani Baba Askofu Shoo, Kaka yangu Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, nimeyasikia yote uliyoyasema kuhusu usalama, amani, umoja na mwendelezo wa Taifa letu, niliamua kunyazama kimya na naendelea kunyama kimya, ninachotaka kuwahakikishia hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza Taifa hili”

“Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye Taifa hili, hayo itoshe kuwa ni ujumbe wangu kwenu, asanteni sana”