JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

WIZARA YA AFYA 

TANGAZO LA UFADHILI WA KUJIENDELEZA KIMASOMO KWA WATUMISHI WA UMMA, KADA ZA AFYA MWAKA 2023/2024 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anawatangazia watumishi wote waliopata udahili wa kusoma masomo ya Shahada ya Uzamili (Masters Degree) katika fani za Afya kwa mwaka 2023/2024 kwamba, Wizara itaanza kupokea maombi ya Ufadhili kuanzia tarehe 11/08/2023 hadi tarehe 07/09/2023. 

Maombi hayo yatawasilishwa kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia ‘link‘ iliyotolewa kwenye tangazo hili. 

Maombi yatakayofanyiwa kazi ni yale yaliyowasilishwa kwa njia ya mfumo huu tu. Hivyo, waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya tangazo hili wanapaswa kufuata utaratibu huu. 

Ufadhili huu ni kwa ajili ya kulipiwa ada ya mafunzo, posho ya kujikimu na nauli (wanafunzi watakaopata ufadhili nje ya nchi), pamoja na posho ya utafiti pindi mwanafunzi anapokuwa kwenye kipindi cha kufanya utafiti kama sehemu ya mafunzo yake. 

Malipo ya posho ya utafiti na posho ya kujikimu yatazingatia viwango vilivyopangwa na Wizara. Vigezo vitakavyotumika kuwapata watakaofadhiliwa ni hivi vifuatavyo : 

1. Kuwasilishwa kwa maombi rasmi ya ufadhili kwa njia ya mfumo (Post-graduate Sponsorship Online Application System) 

2. Mwombaji awe ni Raia wa Tanzania. 

3. Awe mtumishi wa Serikali 

4. Awe ana barua ya udahili kutoka kwenye chuo kinachotambuliwa na Serikali ndani au nje ya nchi 

5. Awe anaenda kusoma masomo ya Shahada ya Uzamili (postgraduate) 

6. Mwombaji awe amethibitishwa kazini (barua ya kuthibitishwa kazini iambatishwe wakati wa maombi) 

7. Ufadhili utazingatia uhitaji unaotokana na uhaba wa taaluma/fani kwenye kituo husika. Kwa mantiki hiyo, kipaumbele cha kupata ufadhili itategemea na upungufu wa taaluma aliyoomba kwenda kusoma kwenye kituo chake cha kazi. 

8. Kipaumbele kitatolewa kwa: 

a. Kuzingatia mpango wa mafunzo wa kusomesha wataalam ulioandaliwa kwa ajili ya kutoa huduma maalum za kibobezi kwenye hospitali za Rufaa za Kanda, Hospitali maalum na Hospitali ya Taifa. 

b. Wataalamu waliopendekezwa na Taasisi zao kwa ajili ya kusoma mafunzo maalumu ya kimkakati ya ‘seti”. 

c. Watumishi wa Serikali ambao baada ya mafunzo watarudi kwenye vituo vyao vya awali au kupangiwa vituo vingine kulingana na uhitaji. 

d. Waombaji waliodahiliwa katika fani ambazo ni za kipaumbele katika utoaji wa huduma za kibingwa. Fani hizo ni 

Anaesthesiology, Psychiatry, Mental health, Clinical Psychology, Occupational Therapy, Rehabilititations Sciences, Paediatrics, Radiology, Surgery, Oncology, Emergency Medicine, Internal Medicine, Orthopaedics Surgery, Otorhinolaryngology, Opthalmology, Haematology, Mental Health, Oral-Maxilofacial Surgery, Dentistry, Orthodentics, Anatomical Pathology, Obstetrics and Gynaecology, Dermatovenereology,Infectious Disese Control, Microbiology and Immunology, Parasitology and Entomology, Critical/Intensive Care Nursing, Cardiovascular Nursing, Oncology Nursing, Nephrology Nursing, Cardiovascular perfusion, Midwifery and Womens Health, Clinical Pharmacy, Pharmaconvigilance, Pharmaceutical Management, Epidemiology and Laboratory Management 

e. Waombaji waliodahiliwa katika nyanja za Ubingwa Bobezi (Super-specialities) zenye umuhimu katika Hospitali Maalumu ili kujenga uwezo wa ndani ya nchi katika jitihada za kupunguza wagonjwa wa rufaa wanaotibiwa nje ya nchi pamoja na kuchochea tiba utalii katika Hospitali Maalum, Kanda na Taifa. Mfano wa taaluma hizo ni 

Neurosurgery, Neurology, Cardiology, Cardiothoracic Surgery, Neonatology, Urology, Plastic & Reconstructive Surgery, Nephrology, Haematology, Pediatric Haemato-oncology, Paediatric Dentistry, Paediatric Oncology, Respiratory Medicine, Endocrinology, Paediatric anaesthesia, Critical Care,Rhinology,Interventional Radiology, Neuroradiology, Pulmunology, Gastroenterology, Interventional Radiography, Medical Imaging, Paediatric Neurology 

f. Waombaji waliodahiliwa kwenye taaluma za kimkakati ambazo mafunzo yake hayatolewi ndani ya nchi kwa mfano, 

Vaccinology, Immunology, Angiology, Feto-maternal Medicine, Gyne-oncology, Surgical Oncology, Pharmacoeconomics, Medical Education, Geriatric Medicine, Mental Health Science, Rehabilitation Science, Adolescent and paediatric psychiatry, Neurosurgery, Bone-marrow Transplant, Cochlea impant, liver transplant, 

g. Waombaji waliodahiliwa katika taaluma za afya za manejimenti na uendeshaji wa huduma za afya kwa mfano, 

Health Monitoring and Evaluation, Health Systems Management, Health Policy and Planning, Health Economics, Health Financing, Health Promotion, Health Laws. 

9. Aidha, mwombaji atatakiwa awe ameambatisha nakala halisi ya nyaraka zifuatazo wakati wa kufanya maombi: 

a. Barua ya ruhusa ya masomo kutoka kwa mwajiri wake 

b. Barua ya udahili kutoka chuoni 

c. Cheti cha taaluma 

d. Cheti cha usajili na Leseni hai kutoka kwenye Baraza la taaluma husika 

e. Cheti cha kuzaliwa 

f. Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Maombi yote yawasilishwe kwa kutumia ‘link’ ifuatayo: https://esponsorship.moh.go.tz/ 

Kama ilivyoelekezwa hapo juu, mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 07/09/2023. 

Imetolewa na: 

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya 

Mji wa Serikali Mtumba Barabara ya Afya, 

S.L.P 743 40478 DODOMA 

11/08/2023