KUMB: PPR/2023 - 08/01 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 2 AGOSTI 2023 news

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 2 Agosti 2023 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama ifuatavyo: Mkoa Petroli Dizeli Mafuta ya Taa TZS/Lita Dar es Salaam 3,199 2,935 2,668 Tanga 3,245 2,981 2,740 Mtwara 3,271 3,008 2,714 

Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yanatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta. 

Bei za mafuta katika miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 1 na bei za mafuta kwa wafanyabiashara wa jumla ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 2. Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 1. Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.


👉BONYEZA HAPA KUONA BEI MPYA YAMAFUTA  news  

AU

👉BONYEZA HAPA KUONA BEI MPYA YA MAFUTA news