JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (MARUDIO) 

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) inawatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye uwezo na sifa za kujaza nafasi za ajira za Kada za Afya 77 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati. Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 09 - 22 Julai, 2023. 

Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa stashahada (Diploma). 

See also: Matokeo Ya Kidato Cha sita 2023/2024 | Form Six Results 2023  news

TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA KADA ZA AFYA 

Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa wanatakiwa kufuata utaratibu ule ule wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha a jira.tamisemi.go.t z. Waombaji ambao waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo huu wanatakiwa kuhuisha taarifa zao na barua za maombi. Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa wanatakiwa kutuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. 

Waombaji ambao waliwahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo huu wanatakiwa kuhuisha (update) taarifa zao na barua za maombi. 


2 1.0 Sifa za Kitaaluma za Waombaji wa Kada za Afya 

1.1 Fundi Sanifu Vifaa Tiba / BIOMEDICAL ENGINEER Daraja la II - TGHS B 

Waombaji wawe na Stashahada ya kawaida ya Ufundi (Full Technician Certificate) ya miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. 

1.2 Fiziotherapia/Mtoa Tiba kwa Vitendo Daraja la II – TGHS B 

Waombaji wawe na Stashahada ya Fiziotherapia/ Mtoa tiba kwa Vitendo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. 


2.0 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI 

Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo: 

i. Awe raia wa Tanzania; 

ii. Awe na umri usiozidi miaka 45; 

iii. Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha Nne, Sita pamoja na cheti cha Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika)

 iv. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali; 

v. Waombaji walioajiriwa kwa mkataba wa ajira kutoka kwa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Afya wanatakiwa kuambatisha nakala za mkataba na barua za uthibitisho kutoka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri husika; 

vi. Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma; 

vii. Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na viii. Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa. 

See also: Matokeo Ya Kidato Cha sita 2023/2024 | Form Six Results 2023  news

3.0 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE 

i. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi katika Halmashauri/Vituo watakavyopangiwa; 

ii. Waombaji wawe tayari kufanya kazi na Mashirika au Taasisi zilizoingia Ubia na Serikali; 

iii. Baada ya kupangiwa kituo cha kazi, hakutakuwa na nafasi ya kubadilishiwa kituo cha kazi; 

iv. Waombaji wote wahakikishe wanajaza taarifa zao na kuambatisha nyaraka zote muhimu kwenye mfumo; na 

v. Maombi ya ajira ni bure. 

4.0 WAHITIMU WALIOSOMA NJE YA NCHI 

i. Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ… kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuwawezesha kuingia kwenye Mfumo wa Ajira; na 

ii. Waombaji waliosoma Vyuo vya Nje ya Nchi wanatakiwa kupata Ithibati ya masomo yao kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili vyeti vyao viweze kutambuliwa na kupata uhalali wa kutumika hapa nchini. Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa maombi, tafadhali bofya: w ww .tami semi.go.tz au wasiliana na Kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba za simu 026 2160210 au 0735 160210. 

Waombaji wenye Ulemavu na sifa zilizoainishwa katika tangazo hili watume maombi yao pia kupitia mfumo. Aidha, maombi yao yaeleze aina ya ulemavu alionao na kuambatisha picha na uthibitisho wa daktari kutoka katika hospitali za Serikali. Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja Ofisi ya Rais - TAMISEMI hayatafanyiwa kazi. Aidha, waombaji watambue kuwa ukishapangiwa kituo hauruhusiwi kuhama au kubadilisha kituo kwa muda wa miaka mitatu.  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 22 Julai, 2023 saa 05:59 usiku. 

Tangazo hili linapatikana katika tovuti ifuatayo: www.tamisemi.go.tz 

Limetolewa na: Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, 

Mji wa Serikali - Mtumba, S.L.P 1923, 41185 DODOMA. 09 Julai, 2023.