JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

OFISI YA RAIS 

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA 

Kumb. Na. JA.9/259/01/A/268                          06/04/2023 


TANGAZO LA KUITWA KAZINI 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 23-24/11/2022, 07-08/12/2022, na 02- 19/02/2023, kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. 

Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana. 

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala yawazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta. 

Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.



JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

  


TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITEnews

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)news



 Leave your comment on our service.....................