Wazazi wakiwa katika hospitali kuu ya Kaunti ya Kakamega kuwajulia hali wanafunzi waliogua baada kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu.


Muktasari:

  • Shule moja Magharibi mwa Kenya imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi wawili kufariki kwa kile kinachodaiwa kuwa walikula sumu kwenye chakula au maji.

Kenya. Shule ya upili ya Mukumu Girls Magharibi mwa Kenya imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi wawili kufariki kwa kile kinachodaiwa kuwa walikula sumu kwenye chakula au maji.

Kwa mujibu wa mtandao wa Tuko wa nchini humo, maofisa wa afya ya umma Jumatatu walifunga, shule hiyo iliyopo kaunti ya Kakamega, baada ya zaidi ya wanafunzi 120 kulazwa hospitalini wiki iliyopita wakiwa na maumivu ya tumbo na kuhara.

Wizara ya Elimu ikiongozwa na mkurugenzi wa Elimu kanda ya Magharibi Jared Otieno imethibitisha kuwa Wizara ya Afya inachunguza kisa hicho ili kubaini chanzo cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa mtandao huo, matokeo ya awali yalionyesha kuwa wanafunzi wanaweza kuwa wamekula sumu kwenye chakula au maji.

Sampuli zilikusanywa na kutumwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (Kemri) kwa uchambuzi.

Shule hiyo imethibitisha kuwa wanafunzi wawili, mmoja kutoka Bungoma na mwingine kutoka Navakholo kaunti ya Kakamega wamefariki kutokana na maambukizi ya bakteria huku ripoti ikisema kuwa Zaidi ya wanafunzi 500 wameathiriwa na bakteria.

Wazazi wamemiminika shuleni kuchukua watoto wao baada ya kupata taarifa kuhusu vifo cha wanafunzi hao wawili.


JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

  


TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITEnews

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)news Leave your comment on our service.....................