Muktasari:

  • Watu 20 wamefariki dunia kufuatia maporomoko ya adhi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kongo. Takribani watu 20 wamefariki baada ya maporomoko ya ardhi kutokea jana Jumapili.

Maafa hayo yalitokea katika Kijiji cha Bulwa katika eneo la Masisi Mkoa wa Kivu Kaskazini. Vyombo vya habari nchini humo, vikiwanukuu viongozi na waangalizi wa eneo hilo, vimesema takwimu za muda zinaonyesha watu wasiopungua 19 wameuawa na msako wa kuwatafuta waathiriwa wengine unaendelea.

Kwa mujibu wa mtandao wa Floodlist, Naibu Kiongozi wa Mkoa wa Kivu Kaskazini, Alexis Bahunga, alitoa taarifa kuhusu hali hiyo katika taarifa aliyoitoa mapema leo.

“Zaidi ya watu 20 wamefariki dunia katika maporomoko ya udongo Jumapili hii tarehe 02.03.2023 huko Bulwa, Gpt Buabo, eneo la Masisi Territory; Ninatoa rambirambi zangu kwa wakazi wa Buabo na ninaiomba Serikali kusaidia familia hizi za waathiriwa kwa kuandaa mazishi ya heshima,” amesema Bahunga katika taarifa.

Pia mvua kubwa imeathiri Mkoa wa Kivu Kusini katika siku za hivi karibuni na barabara inayounganisha mji wa Uvira na Bukavu iligungwa kwa muda.


JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

  


TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITEnews

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)news



 Leave your comment on our service.....................