OFISI YA RAIS 

SEKRETARIETI YA  AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA 

Kumb.Na.JA.9/259/01/A/273                              14/04/2023 

TANGAZO LA KUITWA KAZINI 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 28/09/2022, 25/10/2022, 23-24/11/2022, 08/12/2022, 02-20/02/2023, kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. 

Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana. 

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. 

Asha Rose Migiro, Masjala yawazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta. 

Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. 

Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa. 

NB: 

Waombaji wanaokuja kuchukua barua zao wanatakiwa wawe wamevaa Barakoa na kuja na Kitambulisho kinachotambulika.

👇JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

DAILY JOB VACANCY 06news
DAILY JOB VACANCY 07news
DAILY JOB VACANCY 08 news
DAILY JOB VACANCY 09news
DAILY JOB VACANCY 10news


TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITEnews

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)news


 Leave your comment on our service.....................