Bao la kiungo wa Yanga Mudathir Yahya akiwafunga TP Mazembe limechukua tuzo ya bao bora akiwazidi wenzake watatu.

Mudathir alifunga bao hilo katika ushindi wa kwanza wa Yanga katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mazembe wakati Yanga ikishinda kwa mabao 3-1.

Kiungo huyo alifunga bao hilo la pili katika mchezo huo kwa ufundi akimnyanyulia kipa Narcisse Nlend akipokea pasi ya mshambuliaji Kennedy Musonda.

Katika mchakato wa kura hizo Mudathir amevuna kura 59,357 kati ya kura zote 84,166 sawa na asilima 71.

Mshambuliaji Aymen Mahious wa USM Alger ameshika nafasi ya pili akipata asilimia 21 ya kura zilizopigwa.

Aubin Kramo wa Asec Mimosas ameshika nafasi ya tatu akipata asilima 5 ya kura huku  Paul Acquah wa Rivers United akishika nafasi ya nne kwa asilimia 4.

JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

  


TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITEnews

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)news Leave your comment on our service.....................