Summary

  • Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Yanga  imeeleza kuwa kikosi hicho kwasasa kipo chini ya  Kocha Fredy Mbuna mpaka pale msimu utakapomalizika huku sababu za kuvunja mkataba huo zikiwa hazijawekwa wazi.

BAADA ya Yanga Princess kuonekana kusuasua kwenye Ligi ya Wanawake (WPL) msimu huu hatimaye viongozi wamefikia makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba na Kocha huyo.


Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Yanga  imeeleza kuwa kikosi hicho kwasasa kipo chini ya  Kocha Fredy Mbuna mpaka pale msimu utakapomalizika huku sababu za kuvunja mkataba huo zikiwa hazijawekwa wazi.

"Uongozi wa Klabu ya Yanga unapenda kuutaarifu umma kuwa umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa Timu ya Wanawake, Yanga Princess, Sebastian Nkoma".

Nkoma alitambulishwa rasmi Desemba 10,2022 akitokea Simba Queens na uongozi wa klabu hiyo kufanya uamuzi wa  kumtimua Kocha Mkuu Edna Lema na msaidizi wake Mohamed Hussein 'Mmachinga' baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Fountain Gate Princess.

Kocha huyo aliifundisha Simba Queens kwa mafanikio makubwa na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara mara mbili mfululizo.

Hata hivyo kocha huyo aliondolewa Simba Queens baada tu ya kuipa ubingwa wa Cecafa kwa kuifunga She Corparate ya Uganda bao 1-0  katika mchezo wa fainali uliofanyika Agosti 27.JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 


TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL (New)💥

TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)