Mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Uganda umesimama kwa muda kufuatia taa za uwanjani kupungua mwanga wakati mchezo ukiendelea.

Dakika ya 37 mwamuzi wa mchezo Ibrahim Traore alisimamisha mchezo huo kufuatia hitilafu hiyo huku akiwapa nafasi wachezaji kupata mapumziko mafupi ya kupata maji.

Hata hivyo baada ya wachezaji kumaliza dakika Moja ya kupata maji bado taa hizo zilikuwa hazijarudi katika ufanisi wake zikiwaka chache tofauti na wakati mchezo ulipoanza.

Hali hiyo imeleta sintofahamu kwa mashabiki wanaofuatilia mchezo huo huku maafisa wa mchezo huo wakiwemo waamuzi na mechi kamishna wakijadiliana kusubiri muafaka wa kurejea kwa mwanga zaidi.

Zaidi ya dakika 16 zikitumika kusubiri taa hizo kuongezeka mpaka taarifa hiii ikiandikwa.


JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 


TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL (New)💥

TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)