Summary

  • Yanga ilifuzu robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika huku Simba ikifanya hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa, timu zoe zikiwa na mchezo mmoja mkononi ambapo baada ya kukamilisha hatua hiyo droo itapangwa kujua wapinzani wao kwenye hatua hiyo.

MWANZA. SIMBA na Yanga zinasubiri droo kujua wapinzani wao kwenye robo fainali Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika, lakini Kocha wa zamani wa Mbeya City, Ihefu na Mbeya Kwanza, Maka Mwalwisi amezipa ushauri huku akisisitiza Simba inapaswa kutegua mtego wa kukwama robo fainali.

Yanga ilifuzu robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika huku Simba ikifanya hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa, timu zoe zikiwa na mchezo mmoja mkononi ambapo baada ya kukamilisha hatua hiyo droo itapangwa kujua wapinzani wao kwenye hatua hiyo.

Mwalwisi alisema mafanikio ya klabu hizo ni ya kupongezwa kuanzia wachezaji, makocha, menejimenti na wawekezaji waliofanikisha kupatikana vikosi na mabenchi bora ya ufundi yaliyosaidia kupatikana ubora uliokuwa unatafutwa kwa muda mrefu.

Kocha huyo mwenye leseni A ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) alisema Simba wanahitaji kuvuka hapo walipofikia na kwenda mbele zaidi (nusu fainali) hivyo bila kujali mpinzani na uwanja watakaoanzia mechi wanapaswa kuwa tayari kucheza, kuwaheshimu wapinzani na kutofanya makosa mengi.

“Simba wanalo jukumu kubwa kuvuka hapo wasogee nusu fainali kocha anajua ugumu wa mechi hizi kwahiyo kazi kubwa anayoifanya ni kujaribu kuwatengeneza wachezaji wapunguze makosa mengi ambayo yanaweza kuwaadhibu,” alisema Mwalwisi.

Akiizungumzia Yanga, Mwalwisi alisema wamefikia lengo na hawadai chochote huku akiamini kuwa wakiwaheshimu wapinzani, kutumia akili nyingi kushambulia na kupunguza makosa ambayo wamekuwa wakifanya basi watavuka lengo na kwenda nusu fainali.

“Yanga wamefanya vizuri na wanayo nafasi ya kusonga mbele wanahitaji ubora lakini wasitumie nguvu sana waki-maintain kuwepo robo fainali ni heshima kwao,” alisema Mwalwisi na kuongeza

“Makocha wakifanya maandalizi yao na kuchanga vyema hesabu zao nina imani timu zetu mbili zinaweza kusogea hatua nyingine ya juu zaidi ya hapo na kuleta heshima kwenye ligi yetu,”


JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 


TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL (New)💥

TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)