Dar es Salaam. Licha ya kuwa na kibarua kizito cha hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameanza kupiga hesabu za msimu ujao na kiungo ndilo sehemu la kwanza kuboresha.

Wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa robo fainali, taarifa zinadai kuwa Simba inafanya mawasiliano na wakala wa kiungo wa FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo, Harvy Ossete, ambaye anacheza kikosi kimoja na mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, George Mpole.

Ossete raia wa DR Congo, anatajwa kuwa kati ya viungo ambao wanatazamwa kuwa na sifa ambazo Robertinho anazihitaji kwenye kikosi chake, anaweza kukaba kama ilivyo kwa Sadio Kanoute, kuchezesha timu.

Kwa mujibu wa Mpole, ambaye anacheza kikosi kimoja na mchezaji huyo, alimwelezea Ossete kuwa ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kuisaidia Simba.

Katika wiki hii, Ossete alikuwa sehemu ya kikosi cha DR Congo ambacho kilicheza michezo miwili ya nguvu ya kufuzu kwa Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) dhidi ya Sudan Kusini.


JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

👇👇👇👇👇👇 


TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITEnews

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)news Leave your comment on our service.....................