Katika kuboresha huduma za Afya nchini Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga bajeti ya ununuzi wa magari 727 ya kubebea wagonjwa mahututi yaani (Ambulance) huku magari 214 yakinunuliwa kwaajili ya watumishi wa Afya ili kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.


Naibu Waziri Wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri huk        u akipatia ufumbuzi changamoto zinazowakumba waganga wakuu kwa Niaba ya Waziri Ummy Mwalimu.


“Magari ya kuwasaidia nyie katika Shughuli zenu ni 214 ambazo ni kwaajili ya (RMOs,DMOs) na hakuna wilaya itakosa gari na katika hayo magari mawili yatabaki TAMISEMI na Mengine mawili yatabaki WIZARA YA AFYA na magari 184 yataenda kwenye wilaya zetu kwa waganga wakuu wa wilaya, na magari 26 yataenda kwa waganga wakuu wa Mikoa”.Amesema Dkt.Mollel


Awali akiwasilisha Mwenyekiti wa RMO'S Dkt. Best Magoma akiwasilisha risala yao wameulalamikia Mfuko wa Afya Ngazi ya Jamii (CHF) kutokana na kutokukidhi mahitaji ya wananchi kupata huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchini.


Akijibu risala hiyo, Dkt. Mollel amesema ni kweli kumekua na malalamiko makubwa ya wananchi kutokupata huduma zinazokidhi viwango kupitia kadi za CHF.


"Kila ninapofanya ziara kwenye Mikoa na Wilaya napokea malalamiko juu ya madhaifu makubwa ya CHF na wananchi wanadhani ndio kadi za Bima ya Afya ya Taifa ya (NHIF)”. amesema, Dkt. Mollel.


“Nakiri kuwa CHF ni tatizo kila mahali hata huko nilikofanya ziara wananchi wanalalamikia CHF na wengi wanasema BIMA YA AFYA ukiwambia leteni kadi zenu wanaleta za CHF ambazo siyo NHF”amesisitiza Dkt. Mollel

Dkt. Mollel ametoa wito kwa Waganga wakuu hao kufuata njia muafaka ya kuondokana na kero na malalamiko ya wananchi kwenye upatikanaji wa huduma ni kupitia muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote utaotoa nafasi kwa wananchi kupata huduma bora katika hospitali zote nchini kuanzia zahanati mpaka hospitali ya taifa.


Akizungumzia changamoto ya Uhaba wa Watumishi katika sekta ya Afya Dkt. Mollel amesema hilo ni tatizo la taifa huku serikali ikiendelea kupunguza changamoto hiyo na kutoa rai kwa waganga wakuu hao kuendelea kuajiri watumishi kwa mapato ya ndani.


Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara Afya Dkt. Abel Makubi ametoa rai wa Washiriki wa Mkutano huo kuendelea kupunguza vifo vya mama na mtoto, Kukabili Magonjwa ya TB,HIV na Malaria ambayo yamekua changamoto katika jamii.


“Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya mkayasimamie haya tuendelee kupunguza vifo hivi kwasababu hata Magonjwa yasiyoyakuambukiza yamekua ni tatizo Kadhalika suala la lishe saaa kazi yetu ni kwenda kuhakikisha tunapunguza vifo vya mama na mtoto tuongeze suala la Lishe na mengine tunayatatua ikiwemo suala la chanjo maana kwetu ni kinga madhubuti lazima tuhakikishe idadi ya chanjo inakua juu katika mikoa yetu.” Amesema Dkt.Makubi


Mkutano wa Mwaka wa Waganga Makuu wa Mikoa na Halmashauri unakauli mbiu inayosema Uboreshaji wa Huduma za Afya ni Nguzo ya Kufikia Afya kwa Wote.