JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI 

JESHI LA POLISI TANZANIA 


TANGAZO LA KURIPOTI SHULE YA POLISI MOSHI KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA 

1. Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Nchini kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 31/03/2023 hadi tarehe 07/04/2023 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo. 

2. Vijana waliofanyiwa usaili kwenye Vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi watatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Dodoma tarehe 01/04/2023 saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi. 

3. Vijana waliofanyiwa usaili Mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili tarehe 28/03/2023 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi. 

4. Vijana waliofanyia usaili Makao Makuu ya Polisi Zanzibar wanatakiwa waripoti Makao Makuu Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 28/03/2023 kwa ajili ya kupangiwa utaratibu wa safari. 

5. Aidha, vijana wote waliochaguliwa wanatakiwa waripoti Shule ya Polisi Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo: 

i) Track suti rangi ya blue yenye ufito mweupe, t-shirt nyeupe isiyo na maandishi, raba, soksi nyeusi, bukta za blue kwa ajili ya michezo na mazoezi pamoja na sanduku la chuma (Tranka) la rangi ya blue.

 ii) Chandarua cheupe cha duara na sio cha pembe nne, shuka za light blue jozi mbili (Shuka 4), blanket moja la kijivu lisilo na maua na pasi ya mkaa. 

iii) Vifaa vya usafi: kwanja, jembe lenye mpini, ndoo ndogo mbili, fagio la chelewa. 

iv) Kadi ya bima ya Afya (NHIF) au fedha taslimu Tsh.50,400/= kwa wasio na kadi za bima ya Afya.

 v) Vyeti halisi vya taaluma (Original Academic Certificates), cheti halisi cha JKT/JKU, cheti halisi cha kuzaliwa, kadi ya NIDA au namba ya NIDA, passport size 06 (background blue), na nakala (copy) 5 kwa kila cheti kilichoainishwa hapo juu. 

vi) Fedha ya kujikimu. 


6. Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni, hivyo ni marufuku kuripoti Shule ya Polisi Moshi na simu ya mkononi. Yeyote atakaepatikana na simu itachukuliwa kuwa ni utovu wa nidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano. 

7. Atakaye ripoti Shule ya Polisi Moshi baada ya tarehe 07/04/2023 hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo. 

8. Orodha ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa kwenye tangazo hili. 

Imetolewa na; 

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, 

Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, 

S.L.P 961, 

DODOMA. 

22/03/2023


BONYEZA HAPA KUONA MAJINA
JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 


TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL

TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)


Please leave your comment on our service.......................