Maafisa wa Polisi wakiwa eneo la tukio. Picha na The Mirror.

Muktasari:

  • Takribani watu sita wameuawa kwa shambulizi la risasi lililotokea jana Jumatatu katika Shule ya Msingi Nashville iliyoko Tennessee nchini Marekani.

Watoto watatu na watu wazima watatu wameuawa kwa kushambuliwa kwa risasi wakiwa shuleni na mwanamke aliyetambulika kama Audrey Hale mwenye umri wa miaka 28 nchini Marekani.


Tukio hilo limetokea jana Jumatatu asubuhi katika Shule ya binafsi ya The Covenant, yenye wanafunzi wapatao 200 wanaosoma kuanzia darasa la awali hadi la sita.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vimeripoti kuwa baada ya tukio hilo muuaji ambaye anasadikika kuwa aliwahi kusoma shule hiyo nayeye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi waliofika eneo la tukio.

Idara ya Polisi ya Metropolitan Nashville imetoa taarifa kwamba Hale ambaye ni mkazi wa Nashville alikuwa na bunduki ya kivita na bastola, aliingia ndani ya jengo hilo kwa kufyatua risasi mlangoni.

Polisi waliongeza kuwa Hale alikuwa na ramani za kina za shule hiyo Mkuu wa polisi John Drake aliwaambia waandishi wa habari.


JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 


TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL (New)💥

TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)