Muktasari:

  • Wasanii 10 wa Tanzania wameingia kwenye orodha ya wasanii 25 wa Afrika wanaosikilizwa na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ambaye anatarajiwa kuwasili nchini kesho.

Dar es Salaam. Mtandao wa Spotify umetoa orodha ya nyimbo 25 zinazosikilizwa na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris huku wasanii 10 wa Tanzania wakipamba orodha hiyo ambayo msanii pekee wa kike ni Zuchu kutoka lebo ya WCB.

Harris ambaye yupo barani Afrika ambapo yupo ziarani katika mataifa matatu ikwemo Ghana, Zambia na Tanzania.

Makamu huyo wa kwanza mwanamke katika taifa lenye ushawishi mkubwa duniani, wakati akitarajiwa kuwasili Tanzania kwa ziara yake aliorodhesha baadhi ya nyimbo atakazokuwa akizisiliza katika mtandao wa Spotify huku msanii akishika nafasi ya nane katika orodha hiyo na wa kwanza nchini.

Msanii Hamornize amefungua orodha hiyo kwa Tanzania na nyimbo ya ‘Single Again’ iliyoshika nafasi ya nane, Juma Jux ‘Nice Kiss’ nafasi ya 11, Zuchu ‘Utaniua’, Alikiba ‘Mahaba’, Jay Melody ‘Sawa’ na Mosso ‘Shetani’.

Wasanii wengine wa Tanzania ni Platform nyimbo ya ‘Fall’ Darassa ‘Nobody’ na nyimbo nyimbo ya Marioo akimshirikisha Abbah ‘Lonely’.

Harris katika ziara yake nchini inaelezwa kuwa na umuhimu mkubwa kutokana na ushirikiano wa muda mrefu ambao umeiwezesha Tanzania kunufaika na uwekezaji na misaada kutoka kwa watu wa Marekani.

Makamu huyo anatarajiwa kuwasili kesho Machi 29, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINA) atapokelewa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dk Philp Mpango.

Pia, Alhamisi Machi 30, Harris atakutana na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo wawili hao watakuwa na mazungumzo kabla ya jioni yake kushiriki Futari itakayoandaliwa Ikulu.



JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES.

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 



TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL (New)💥

TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)