Summary

  • Hadi sasa KMC ipo nafasi ya 12 na alama 26 kati ya timu 16 za Ligi Kuu lakini bado haijajihakikishia nafasi ya kusalia kwani inahitaji ushindi kwenye mechi walau tatu ili kufanikisha hilo kutoka na ushindani uliopo.

KMC juzi ilikuwa uwanjani ikicheza mechi ya kirafiki na Azam fc lakini bado haijawa na uhakikika wa kusalia Ligi Kuu kutokana na namna msimamo ulivyo hadi sasa ikiwa imebakiza mechi tano tu kumaliza msimu lakini mastaa wa timu hiyo wameahidi kupambana na kuhakikisha timu haishuki.

Hadi sasa KMC ipo nafasi ya 12 na alama 26 kati ya timu 16 za Ligi Kuu lakini bado haijajihakikishia nafasi ya kusalia kwani inahitaji ushindi kwenye mechi walau tatu ili kufanikisha hilo kutoka na ushindani uliopo.

Wakizungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti, viungo wa timu hiyo, Baraka Majogoro na Stive Nzigamasabo wamesema wanajua ugumu wa mechi za lala salama lakini wapo tayari kupambana ili kuhakikisha timu inamaliza msimu ikiwa sehemu salama zaidi.

"Mechi za mwisho zinakuwa ngumu sana kutokana na kila timu kutaka kutimiza malengo yake. Hata sisi pia tunataka tufikie malengo hivyo tupo tayari kupambana  katika mechi zijazo ili kuhakikisha hilo linatimia," alisema Majogoro.

"Naamini hatutashuka daraja, tuna uwezo wa kufanya vizuri katika mechi zilizobaki na kumaliza ligi tukiwa sehemu nzuri," alisema Nzigamasabo aliyekuwa kwenye timu ya taifa ya Burundi katika mapumziko haya.

KMC kwa sasa imebakiza mechi na Geita Gold, Dodoma Jiji, Singida Big Stars, Tanzania Prisons, na Mbeya City.


JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 


TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL (New)💥

TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)