Pep Guardiola ni kocha aliyefanikiwa sana kwenye mpira. Katika misimu yake 13 kwenye ligi kuu mbali mbali, ameshinda ubingwa mara 10.

Labda nianze kwa kuwatambulisha watu niliowataja hapo juu ili tuelewane kuanzia mwanzo.

Genevieve Nnaji ni mmoja wa nyota wakubwa sana wa kike wa filamu kutoka Nigeria, nchi kinara wa filamu Afrika.

Ameshinda tuzo nyingi za ndani ya Nigeria, Afrika na duniani kwa ujumla.

Filamu yake ya Lionheart ndiyo ya kwanza kutoka Nigeria kuingia kwenye Netflix na ndiyo filamu ya kwanza kutoka Nigeria kuwania tuzo za Oscar.

Genevieve Nnaji ni msanii mkubwa sana. Nasreddine Nabi ni kocha wa klabu ya Yanga. Ni kocha anayetajwa kama kocha bora Tanzania kwa sasa.

Ameiongiza Yanga kuweka rekodi ya kucheza mechi 49 bila kupoteza huku ikipiga soka la maana.

Ameiongoza Yanga kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na kuvuka hadi robo fainali. Nabi kocha bora Sana kwa sasa hapa Tanzania.

Sasa chukulia Nabi ni shabiki mkubwa sana wa Genevieve na fumba fumbua muigizaji hiyo anakuja Tanzania.

Nabi matarajio yake kumuona Genevieve kwenye mechi ya Yanga, ghafla anasikia alienda kwenye mechi ya Simba.

Hiki ndicho kilichomtokea Pep Guardiola, kocha wa Manchester City ya England.

Raia huyo wa Hispania ni shabiki mkubwa sana wa msanii wa filamu kutoka Marekani, Julia Roberts.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Leipzig, Pep Guardiola alielezea kusikitishwa kwake na muigizaji huyo.

2016 Julia Roberts alienda England na akatembelea Old Trafford, uwanja wa Manchester United.

Pia alitembelea Stamford Bridge, uwanja wa Chelsea na kupata nafasi ya kuongea na kocha wa wakati huo, Antonio Conte. Hii aliiongea Conte mwenyewe akimjibu Pep.

Sasa kumbe ile ziara ya Old Trafford ilimuumiza sana Pep na akaliweka moyoni hadi juzi kati hapa ndiyo akalitoa, baada ya City kushinda 7-0 na nyota wao Erling Haaland kufunga mabao matano peke yake.

Hata kama nitashinda ubingwa wa Ulaya mara tatu mfululizo bado nitakuwa nimefeli.

“Nina mashujaa watatu katika maisha yangu. Michael Jordan, Tiger Woods, na Julia Roberts. Hawa ni mashujaa wangu watatu.

Julia Roberts miaka kadhaa iliyopita alikuja Manchester - siyo ile miaka ya 90 wakati Sir Alex [Ferguson] alikuwa akishinda mataji na mataji na mataji.

Alikuja katika kipindi ambacho sisi tulikuwa bora kuliko United, katika miaka hii minne au mitano, sawa?

“Na alienda kuwatembelea Man United. Hakuja kutuona sisi. Hiyo ndiyo maana nasema hata nikishinda ligi ya mabingwa haitokuwa sawa na kitendo cha Julia Roberts kuja Manchester na hakuja kutuona sisi”.

Pep Guardiola ni kocha aliyefanikiwa sana kwenye mpira. Katika misimu yake 13 kwenye ligi kuu mbali mbali, ameshinda ubingwa mara 10.

Ameshinda kila lombe ambalo ameshindania lakini anakuwa mdogo kwa kutotembelewa na Julia Roberts.

Sasa najaribu kuileta katika mazingira ya nyumbani.

Genevieve Nnaji aje Tanzania na aende kuwatembelea Simba, je Nabi ataumizwa kama Pep?

Hakuna anayeweza kuwa na jibu la swali hili zaidi ya Nani mwenyewe, lakini mfuatiliaji wa mambo ya Afrika anaweza kuhisi jibu.

Tofauti na Ulaya, Afrika tuna mipaka mikubwa sana.

Yaani tamaduni za nchi zetu zina muingiliano mdogo sana. Japo Nani ana uraia wa Ubelgiji lakini kutokana na asili yake ya Tunisia, anaweza asimjue kabisa Genevieve.

Tofauti na wenzetu Magharibi japo kila nchi ina mambo yake ya ndani, lakini tamaduni zao zimeingiliana sana kiasi kwamba msanii mkubwa wa nchi moja ni maarufu Ulaya yote...hadi Marekani.

Ndiyo maana Pep anaumizwa na Julia Roberts, lakini Nabi ni vigumu sana kuumizwa na Genevieve.

Unaweza kusema Nigeria mbali, tuzungumzie wasanii wetu wa ndani...labda Irene Uwoya, Nani ndiyo kabisa anaweza asimjue...au kama anamjua labda baada ya kuona ile picha aliyopiga na Mayele kwenye like tangazo la biashara.

Afrika ina nchi 54, kama zote zingekuwa na muingiliano wa kiutamaduni na zilivyo nchi za Magharibi, tungefanikiwa sana.

Watu zaidi ya bilioni moja wa Afrika ni mataji mkubwa sana endapo wote wangekuwa na muingiliano...maana yake msanii mkubwa wa Tanzania anakuwa mkubwa Afrika nzima.

Msanii mkubwa kwa watu bilioni moja, huyo ni tajiri sana.

Mtu anaweza kutaja changamoto ya lugha, lakini hiyo siyo Afrika tu...kote kuna changamoto ya lugha, hata Ulaya.

Lakini nguvu ya tamaduni imepunguza ukubwa wa mipaka na kuvunja kizuizi cha lugha na kuacha sanaa itembee.

Ndiyo maana hata vilabu vyao vya michezo vinapata mashabiki kila sehemu.

Hapa Afrika, Al Ahly ya Misri na ukubwa awake wote, ikija Tanzania haipati mashabiki.

Itokee mechi ya Al Ahly na Zamalek uwanja wa Mkapa, watu hata robo ya uwanja hawaendi.

Ni kwa sababu nguvu ya Al Ahly na Zamalek iko Misri tu, haivuki mipaka...hivyo hivyo kwa Sanaa nyingine.

Ni mara chache sana sanaa kama muziki imefanikiwa kupunguza ukubwa wa mipaka...lakini sanaa zingine bado sana.

Ndiyo maana Nabi hawezi kuumizwa na Genevieve



JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR MORE UPDATES

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 






TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL (New)💥

TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE

TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)