JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

OFISI YA RAIS 

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA 

Kumb.Na.JA.9/259/01/A/250                 19 MACHI, 2023 TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 26 hadi 27 Machi, 2023 nahatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:- 

i. Usaili utafanyika tarehe 26 hadi 27 Machi, 2023 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada; 

ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa, 

iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; 

iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:-Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria; 

v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzi acheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji; 

vi. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatizamatokeozakidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI; 

vii. Kila msailiwa atajigharamia Chakula, Usafiri na Malazi; 

viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili; 

ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA); 

x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika. 

xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi. 

xii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwakuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili. 
RATIBA YA USAILI

👇👇👇👇👇👇JOIN OUR SOCIAL MEDIA PLATFORMS FOR DAILY UPDATES

JOIN OUR WHATSAPP GROUP  

👇👇👇👇👇👇 


TAP HERE TO JOIN OUR TELEGRAM CHANNEL


TAP HERE TO VISIT OUR WEBSITE


TAP HERE TO DOWNLOAD OUR APP (GOOGLE PLAY STORE)


Please leave your comment .................