Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya Dakar nchini Senegal tarehe 25-27 Januari, 2023 katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Januari, 2023.

Mhe. Hussein Bashe amejibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya mikutano ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyohudhuria hivi karibuni nchini Senegal kusiana na sekta ya Kilimo.

Waziri Bashe amewahakikishia watanzania kuwa nchi iko salama na kwamba serikali itaendelea kuhakikisha mkulima anafaidika na kazi ya kilimo anayofanya.