JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS 

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na. JA.9/259/01/A/220                         08 Februari, 2023


TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala Wa Serikali (MDA's) na Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA's), anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 13 – 20 Februari, 2023 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. 

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:- 

i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 13 – 20 Februari, 2023 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada; 

ii. Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa mchujo na Vitendo, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya kazi; 

iii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa;

iv. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; 2 

v. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria; 

vi. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji; 

vii. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI; 

viii. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi; 

ix. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili; 

x. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA); 

xi. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika. xii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni zakufanyia kazi.



👇👇👇👇👇👇