Company Description
The uniquely fertile area surrounding Mount Kilimanjaro, in Tanzania, is among the best regions in the world for the cultivation of Arabica, the queen of the coffee beans. Such a high-quality product naturally incurs high demand. For this reason, Kilimanjaro Plantation has set itself three challenging targets:
- We aim to produce the best Highland Arabica coffee in Tanzania.
- We aspire to remain a reliable and long-standing partner for coffee connoisseurs of all kinds.
- We strive to harmonize our quality with the environment and people - we guarantee strict adherence to social, cultural and environmental guidelines and regulations.

 

Job Details

Kilimanjaro Plantation Limited (KPL) ni kampuni inayozalisha kahawa yenye sifa nzuri ndani ya Mkoa huu. Dhamira yetu kuu ni kuzalisha Kahawa ya Arabika iliyosafishwa kwa ubora wa juu kabisa nchini Tanzania. Mafanikio ya Kampuni yamechangiwa na kujitolea kwake kwa utumishi, pamoja na kuajiri na kufanya wafanyakazi wenye uweledi na waadilifu kudumu katika kazi. Kilimanjaro Plantation Limited inatoa ajira za kimkataba kwa nafasi ya kazi ifuatayo.

 

ULINZI (NAFASI 10)

Kilimanjaro Plantation Ltd (KPL) inatarajia kuajiri walinzi watakaofanya kazi katika maeneo mbalimbali ya kampuni.

WIGO WA KAZI

Mlinzi atafanyakazi kwa ukaribu na Mkuu wa Idara ya Ulinzi, Wasimamizi wa Ulinzi, Meneja wa shamba, Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu & Sheria na/ama Mkurugenzi Mkuu katika kampuni ya Kilimanjaro Plantation Ltd.

SIFA NA UZOEFU KWA MWOMBAJI

a)       Awe amepitia Mgambo

b)      Awe ni raia wa Tanzania

c)      Awe na umri kuanzia miaka 25 hadi miaka 45 na sio zaidi

d)      Barua ya utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Kata au Kijiji

e)      Awe ameambatanisha Namba ya Mlipa Kodi (Tin Number)

f)       Awe mwaminifu na mwadilifu na asiwe amewahi kufungwa jela au kuhukumiwa kwa makosa ya jinai.

g)      Awe na uzoefu na kazi ya ulinzi

h)      Awe na kitambulisho cha taifa(NIDA) au namba ya NIDA

i)        Barua yake ya maombi iwe na wadhamini wasiopungua wawili wakiwa na picha na pamoja na vitambulisho vyao.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:

Waombaji wote watahitajika kutuma maombi yao kwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu & Sheria na kwa barua pepe wakiambatanisha nyaraka zifuatazo; Barua ya maombi ya kazi, Wasifu wa Mwombaji (CV), Vyeti vya taaluma na fani, picha ndogo 1 (passport size) na barua ya utambulisho kutoka kwenye serikali ya mtaa kupitia barua pepe: [email protected]au kwa njia nyingine, kuwasilisha maombi kwa mkono katika anwani ilitolewa hapo chini;

Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu & Sheria;

Kilimanjaro Plantation Ltd;

S. L. P 976;

Moshi, Kilimanjaro.

 

MUHIMU:
Maombi yatatakiwa kuwasilishwa kabla ya tarehe 16.02.2023 saa 09:00 jioni. Waombaji waliopitishwa tu ndio watakaoitwa kwenye usahili baada ya tarehe ya mwisho ya kutuma maombi.