MABADILIKO YA KUMBI ZA USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwatangazia wasailiwa wote waliofaulu usaili wa kuandika (mchujo) na waliochaguliwa kuhudhuria usaili wa mahojiano (ana kwa ana) kwa nafasi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kuwa usaili wa mahojiano utafanyika katika kumbi za Shule ya Sekondari Dodoma iliyopo Makole - Shirika la Nyumba la Taifa karibu na soko la Sabasaba la jijini Dodoma.

Hivyo kufuatia mabadiliko haya wasailiwa wote waliochaguliwa kuhudhuria usaili huo wanapaswa kuzingatia tarehe za saili hizo kulingana na kada kama zilivyoelekezwa katika tangazo la awali lenye Kumb. Na. JA.9/259/01/A/2012 la tarehe 20 Januari, 2023.