Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetoa taarifa rasmi ikiwa zimesalia siku chache kuelekea kuanza kwa michuano ya Kimataifa ngazi ya vilabu.

CAF wametoa taarifa kuwa vilabu sasa vinaruhusiwa kuingiza mashabiki kwa idadi ya uwanja husika pasipo kuomba ruhusa tena kutoka CAF kutokana na zuio walilokuwa wameweka sababu ya Corona.

Awali CAF walikuwa wanaruhusu 15% hadi 30% ya mashabiki waingie uwanjani kwa sharti la club kuomba mapema lakini sasa hivi mambo yamerudi kama zamani hivyo Simba na Yanga kwa Tanzania watakuwa na nafasi ya kujaza mashabiki katika mechi zao.